Published on

Jinsi ya kutumia AI kuanzia ideation phase hadi deployment phase

Authors
  • avatar
    Name
    Godbless Nyagawa (Njox)
    Twitter
    @njox16

Kumekuwa na AI bubble…

Kuanzia 2022, dunia ya tech imejaa AI kila kona. Lakini je, unaweza kutumia hizi AI tools kama developer wa Bongo kwenye kazi zako za kila siku? Leo naangazia tool moja ya kipekee ambayo inaweza kukusaidia kuanzia idea hadi project ikawa live na launched.

Tool Hiyo Ni Ipi?

Sio nyingine bali ni ChatGPT kutoka OpenAI. Kuna stages nyingi ambazo developer hupitia kwenye kutengeneza project — kuanzia ideation, setup, UI/UX, backend, integration, testing, deployment, na polishing.
Na guess what? ChatGPT anaweza kushika mkono wako kwenye kila hatua.


🛠️ REAL EXAMPLES: ChatGPT in Action

Nitakuonyesha namna ChatGPT anavyoweza kusaidia kwenye kila hatua:

✅ Planning & Scoping

Hapa ndio unaanza kuspecify idea yako. Unaandika features, unaamua tech stack, na una-scope user flow zako.

Prompts:

> Summarize pros/cons of using MongoDB vs PostgreSQL for this project.
> Write a spec for an admin dashboard with 3 user roles.
> Give me 5 MVP feature ideas for a SaaS to manage university keys.

🏗️ Architecture & Setup — ChatGPT kama Tech Lead

Hapa unajenga msingi wa nyumba yako (project). Folder structure, database design, roles, na decisions za infra.

Prompts:

> Generate a folder structure for a MERN stack SaaS with auth and admin panel.
> Design a MongoDB schema for bookings, users.

👨‍💻 Development — ChatGPT kama Coding Pair

Unashuka mzigoni sasa. Unaandika routes, components, APIs, na hata kufix bugs.

Prompts:

> Explain this error: TypeError: Cannot read properties of undefined.
> Write an Express route to return weekly booking stats grouped by venue.

🧪 Testing & QA — ChatGPT kama Bug Exterminator

Kuandika tests sio mchezo, lakini AI inaweza kusaidia kuandika test cases, kufix flaky tests, na kusuggest edge cases.

Prompts:

> Write a unit test for a login function in Node.js using Jest.
> List common edge cases when a user submits a booking form.

🚀 Deployment — From Localhost to Live

Project yako ikishakamilika, sasa ni wakati wa kuipeleka hewani. ChatGPT anasaidia kuandika Dockerfile, CI/CD configs, na hata ku-deploy via GitHub Actions.

Prompts:

> Write a Dockerfile for a Node.js app using MongoDB.
> Explain how to set up GitHub Actions to deploy to Vercel on push.

🏁 Mwisho wa safari?

Hapana. After deployment unarudi tena kwenye feedback, performance improvements, scaling — rinse & repeat.

Ikiwa unataka full PDF ya AI prompts hizi zote kwa kila hatua, click link hapa chini:

👉 Link ya kupakua


Pro Tip: Usione ChatGPT kama assistant tu — treat it like your co-founder in code, especially kama unajenga solo. Hii ndio dev superpower ya 2025.

Stay building. — Njox 👨🏾‍💻